Matokeo chanyA+ online




Wednesday, May 12, 2021

WAZIRI JAFO ASHIRIKI FUTARI NA WATUMISHI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi hao katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, iliyofanyika jijini Dodoma ambapo aliwaasa Watanzania kuliombea Taifa liendelee kuwa na Amani.

Pia aliwataka watumishi hao kuendelea kudumisha upendo na kuwasaidia wananchi wanawahudumia ambapo pia alitumia nafasi hiyo atakiwa heri katika Mfungo Mtukufu wa Ramadhani kuelekea Sikukuu ya Eid el Fitr.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (katikati) akiwa na watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa futari iliyoandaliwa Jafo ametoa wito huo  Mei 11, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akiwaongoza watumishi wa Ofisi hiyo katika hafla ya futari kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga  akipakua futari wakati wa hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi wa Ofisi hiyo ikiwa ni sehemu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi wa Ofisi hiyo jijini Dodoma Mei 11, 2021.

Kiongozi wa dini ya Kiislamu akiomba Dua kwa ajili ya hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais iliyoafanyika jijini Dodoma Mei 11, 2021.

No comments:

Post a Comment