Matokeo chanyA+ online




Saturday, January 13, 2018

DOLA ElFU 83 ZAKAMTWA UWANJA WA NDEGE WA MWL NYERERE


Tarehe 13/01/2018 majira ya saa 15:30hrs Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere eneo la juu la kuondokea abiria Terminal II, maafisa wa Forodha wakishirikiana na Polisi JNIA na maofisa wa usalama walimkamata abiria aitwae Boniface s/o Aldo Mbilinyi, Mtanzania mwenye hati ya kusafiria nambari AB 757247, Kabila Mbena, umri miaka 32, kazi Biashara na Mkazi wa Tabata Segerea aliyekuwa akisafiri na ndege ya shirika la ndege la Emirate kuelekea Dubai akisafirisha Dola za kimarekani 123,000.
Abiria alitoa taarifa TRA (self declaration) ya dollar 40,000 tu ambayo ni pungufu ya (USD) 83,000.00 ambazo hakuzitolea taarifa. Abiria huyo alikuwa alielekea Dubai kwa safari ya kibiashara.Kiasi cha pesa ambazo hazikututolewa taarifa (USD 83,000.00) tume seize na ku deposit kwenye akaunti ya Dollar ya FIU number 20110028135.
Abiria (mtuhumiwa) anashikiliwa na jeshi la polisi (Termina One) kwa mahojiano zaidi




No comments:

Post a Comment