Serikali imeendelea kufanya kazi ya
Uendelezaji wa Viwanda ambapo kazi zilizotekelezwa ni upanuzi wa Kiwanda
cha Ngozi na Bidhaa za Ngozi cha Karanga (Moshi) na kuimarisha Shirika la
Nyumbu (Pwani) ili kuongeza uzalishaji ikiwemo magari ya zimamoto.
![]() |
Bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda cha Karanga |
Hayo yemesemwa na
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango katika taarifa yake ya mapendekezo
ya Serikali ya mpango wa maendeleo wa taifa na ya kiwango na
ukomo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21 mjini Dodoma.
Waziri Mpango amesema kuwa serikali pia imefanyia kazi ya kufutwa na kupunguzwa kwa ada na tozo
54 ili kuondoa kero na urasimu kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini.
Aidha ameongeza kuwa kuzinduliwa
na kuanza uzalishaji katika viwanda saba (7) ambavyo ni kiwanda cha Pipe
Industries Co. Limited (Dar es Salaam), kiwanda cha chai cha Kabambe (Njombe),
kiwanda cha Yalin Cashewnut Company Ltd (Mikindani – Mtwara), kiwanda cha 21st
Century Food and Packaging (Dar es Salaam), kiwanda cha kusaga mahindi cha
kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited – MeTL (Dar es Salaam), kiwanda
cha bidhaa za plastiki cha Plasco Pipelines Co. Ltd (Dar es Salaam), kiwanda
cha kupakia na kuhifadhi parachichi - Rungwe Avocado (Mbeya) na kiwanda cha
kuchakata parachichi kwa ajili ya kutengeneza mafuta (KUZA Afrika).
Ambapo amesema kuwa jumla ya tani 4,254.1 za korosho zilibanguliwa kupitia viwanda 17 na kuwezesha
kuzalishwa kwa fursa za ajira za moja kwa moja 4,066, Na kwa kipindi cha mwaka 2016/17 -
2019/20, jumla ya viwanda vikubwa 201, vya kati 460, vidogo 3,406 na vidogo
sana 4,410 vilianzishwa.
No comments:
Post a Comment