Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa Serikali imendelea kukarabati reli ya kati ikijumuisha njia
ya reli, madaraja na ujenzi wa makalavati kwa vipande vya Dar es Salaam
– Ngerengere (km 145) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 89.14.
Aidha amesema kuwa kwa upande wa Ngerengere -
Kilosa (km 138) ujenzi umefikia asilimia 59.43, ambapo Kilosa - Itigi (km 343) ni asilimia 82.57 na Itigi
- Isaka (km 344) umefikia asilimia 82.05.
Akizungumzia ukarabati wa reli ya Tanga – Arusha (km 439)
amesema kuwa ujenzi umeendelea ambapo ukarabati wa kipande cha reli ya Tanga – Moshi (km 353)
umekamilika na kuanza kusafirisha abiria na mizigo ambapo ukarabati wa kipande cha
Moshi – Arusha (km 86) umeendelea kwa kubadili reli na mataruma na kurejesha
madaraja na makalavati, kukarabati stesheni na kufungua mifereji ya maji ya
mvua ambapo utekelezaji umefikia asilimia 90
No comments:
Post a Comment