Matokeo chanyA+ online




Thursday, December 31, 2020

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, KHAMIS HAMZA CHILO AKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI MKOA WA KUSINI PEMBA

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo (aliyevaa tai), akikagua matofali ya Ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi, zilizopo eneo la Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba, wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi huo leo, lengo ikiwa ni kutatua makazi ya askari hao.Kushoto ni Kamishna wa Jeshi la Polisi  Zanzibar, Mohammed Haji Hassan.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mohammed Haji Hassan (wapili kushoto),akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo wakati wa ziara ya ukaguzi  wa  Mradi wa Ujenzi wa  Nyumba za Makazi ya Askari Polisi,leo  zilizopo eneo la Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment