Matokeo chanyA+ online




Thursday, May 5, 2022

KILO 22,800 ZA MATUNDA YA PARACHICHI KUTOKA TANZANIA ZAWASILI INDIA KUFUNGUA SOKO KUBWA LA ZAO HILO NCHINI HUMO

 

Tarehe 4 Mei 2022 ni siku adhimu ambapo kwa mara ya kwanza Ubalozi wa Tanzania nchini India, umepokea Kontena la maparachichi kutoka Tanzania kupitia Kampuni ya IG Fruits ya nchini India. Mapokezi haya yamefanyika katika Bandari ya Jawaharlal Nehru Mumbai.
 
‘Naomba kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu maparachichi tuliyoyapokea leo ni Kontena la futi 40 ambalo ndani yake lina trays za parachichi 5,700. Na kila tray moja lina uzito wa kilo 4. Huko nyuma tuliwahi kupokea shehena ya kilo 200 ambayo ilikuja na ndege yetu ya ATCL’ - Balozi Anisa K Mbega
 




 

No comments:

Post a Comment