Matokeo chanyA+ online




Tuesday, April 25, 2023

KLINIKI YA AGA KHAN, MKOA WA MJINI MAGHARIBI.



Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amesema Shirika la maaendeleo la Aga Khan (AKDN) limekuwa likijitahidi kuimarisha afya na ustawi wa jamii ulimwenguni kote pamoja na Zanzibar. Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 25 Aprili 2023 katika uzinduzi wa kituo cha afya cha Kliniki cha Aga Khan ambacho kitatoa huduma za dharura, huduma za kibingwa pia wagonjwa watapata huduma za afya zilizounganishwa dijitali na Hospitali ya Aga Khan iliyopo Dar es Salaam. Serikali ya Zanzibar inatambua umuhimu wa huduma bora za afya hivyo sekta hiyo imepata mageuzi makubwa ambayo yanajumuisha huduma za afya kwa ngazi ya shehia, wilaya hadi mkoa kupitia Hospitali za rufaa ikiwa na jumla ya vituo vya afya 172 ambavyo vipo katika wilaya 11 Zanzibar. Naye Binti Mfalme Zahra Aga Khan alisema uwekezaji kupitia Shirika la maendeleo la Aga Khan kupitia miundombinu ya huduma za afya ya Zanzibar inaonyesha dhamira yake ya kuendelea kuboresha afya na ustawi wa jamii ulimwenguni kote.

No comments:

Post a Comment