Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cook |
Hayo yamebainika leo wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu na
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cook aliyemtembelea ofisini
kwake jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho pamoja na kuzungumza kuhusu ushirikiano
na uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili Waziri Zungu akifafanua alisema kuwa
Mkutano huo Tanzania itatoa mchango wake wa namna inavyopambana na changamoto
hii ya kimazingira.
“Tumezungumza hasa uhusiano mzuri tulionao na nchi hiyo
lakini pia kuhusu mkutano utakaofanyika Glasgow na tunatakiwa tutoe vipaumbele
vyetu vya namna Tanzania itasaidiaje kuokoa mazingira kiulimwengu, namna gani
inadhibiti hewa ya ukaa isizagea katika maeneo mengine,” alisema.
Waziri Zungu alibainisha kuwa watalamu wanakaa kwa ajili ya
na kushughulikia vipaumbele kuhusu hatua za kuchukua katika mabadiliko ya
tabianchi ili vipitishwe na mamlaka zinazohusika kabla ya kuwasilishwa kwenye
mkutano huo.
Kwa upande wake Balozi Cook aliipongeza Serikali ya
Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa hatua zake katika kupambana na
uharibifu wa mazingira pamoja na changamoto zilizopo.
Alisema kuwa mkutano huo utasaidia nchi zinazoendelea
ikiwemo Tanzania ambazo zinaathirika na mabadiliko ya tabianchi kuwa na fursa
ya kupata misaada ya kifedha kwa ajili
ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
“Kiukweli mabadiko ya tabianchi yanaathiri sana wananchi
hasa wakulima wanashindwa kuwa na kilimo cha ukakika kwani hali ya hewa
haitabiliki hivyo tumejipanga kutoa elimu ili kukabiliana na changamoto hiyo,”
alisema.
No comments:
Post a Comment